Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 28 Februari 2014

Hoja ya Mh. Mbatia yamkuna mwenekiti wa mda Mh. Pandu Ameir Kificho wa bunge maalum la katiba

Ilikuwa ni hoja ya kibusara ambayo ilichangiwa na Mh. Mbatia wakati wa Taswira ya Bunge maalum hapo jana. Mh. Mbatia aliwasihi wajumbe wote kutumia hekima na busara katika kuendesha na kutoa maoni juu ya uchambuzi wa rasimu ya pili ya katiba. Aliwaomba wajumbe kuwa na focus ya pamoja na kuacha malumbano yasiyojenga umoja ndani ya wajumbe, kwani alidai kuwa wajumbe wako pale kwa kazi ya kuchambua katiba ya watanzania wote na sio kwa maslahi ya vyama vya siasa na makundi ya kidini. 

Hoja hiyo ilimgusa mwenyekiti wa mda Mh. Pandu na kuwasihi wajumbe wote kuufanyia kazi ushauri huo.

Picha hizi baadhi ya wajumbe waliochangia hoja jana, bungeni kwenye semina hiyo.Hakuna maoni: