Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 28 Februari 2014

Mjadala bungeni juu ya Rasimu ya pili ya katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tz

Jana tarehe 27.2.2014 ilikuwa ni siku nyingine ambapo wabunge maalum wa bunge la katiba mpya wamejadiliana juu ya sheria na taratibu za kuliongoza bunge maalum wakati wa shughuli nzito ya kuchambua na kuandaa katiba mpya.

Baadhi ya wajumbe walishiriki kutoa maoni, mapendekezo ya nikwa namna gani mchakato mzima wa shughuli bungeni ziendeshwe. Katika hoja na mitizamo mingi ya wabunge ilionekana kutofautiana juu ya kipengele cha kupiga kura baada ya makusanyo, mapendekezo na mapitisho ya mijadara na maoni ya wajumbe wote bungeni kupitia kamati maalum iliyoteuliwa na bunge kushughurikia maoni na mapenekezo ya wabunge.
 
Katika tofauti za hoja za wabunge, baadhi walionekana kuunga mkono kura za siri na huku wengine wakipendekeza kura za wazi (dhahiri). Mbali na hayo, katika utoaji wa hoza hizo kinzani, baadhi ya wajumbe walionekana kutoa hoja zao kwa hisia kali na kana kwamba wanatishiana.

Lakini kwa mantiki ya kawaida, kulingana na mchakato mzima wa kuchambua rasimu hiyo inaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia na inafanyika pasipo na usiri wowote, kwani mijadara huoneshwa kwenye vyo mbalimbali vya habari, itakuwa vyema endapo kura zitapigwa dhahiri (wazi). Na mantiki ya kudai kwamba kura zipigwe kwa usiri kama walivodai baadhi ya wajumbe wa bunge, kuwa ni utaratibu wa mda mrefu na kila bunge la katiba kokote duniani hufanya vile, nadhani sio razima sana, kwani sisi watanzania tunataka kuona wajumbe wapige kura dhahiri pasipo kuogopa mtu mwingine ili kuweza kukomaza demokrasia ndani ya Nchi yetu toka bungeni na kwa Nchi nzima

Hakuna maoni: