Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 18 Aprili 2015
AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2015
Kwa kawaida upangaji wa walimu ajira mpya hufanywa na OWM TAMISEMI baada ya kupokea arodha ya walimu kutoka katika vyuo na  vyuo vikuu kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi baada ya kuhitimu na kufuzu kozi zao. Hata hivyo upangaji huo unatakiwa  kuzingatia dhamira ya serikali ya kuleta usawa kwa kupanga walimu kwenye halmashauri mbalimbali kulingana na mahitaji. Ili kuhakikisha kuwa kuna usawa, serika;li kupitia OWM TAMISEMI na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilifanya ufuatiliaji wa kina hadi ngazi ya shule kubaini kwa uhakika zaidi mahitaji halisi ya walimu kwa kila halmashauri na kila shule. Ufuatiliaji huo umebaini kuwepo kwa halmashauri na shule hasa za mjini zenye walimu wa ziada nazingine hasa za vijijini ambazo zina upungufu mkubwa wa walimu. Napenda kuwaarifu kuwa taarifa hizo zimetusaidia kuwapanga walimu wapya kwa usawa na haki ili kuondoa uwiano usio ridhisha kwenye maeneo mengi ya vijijini. Hivi sasa tunakamilisha taratibu mahususi za kupata kibali kwa ajili ya ajira za walimu na upatikana wa fedha za kuwalipa stahili zao zinakamilishwa ili kuwezesha walimu wapya kuanza ajira rasmi ifikapo tarehe 1 Mei, 2015. Napenda kuweka bayana kuwa Maeneo mengi ya mijini kwa maana ya Majiji, Manispaa na Miji hayajapangiwa walimu na baadhi yamepangiwa walimu wachache kulingana na mahitaji. Kama nilivyoeleza hapo awali kipaumbele kimetolewa katika maeneo ya vijijini na halmashauri ambazo zina upungufu mkubwa wa walimu.Nawashauri na kuwasihi walimu wapya waende kuripoti kama halmashauri na shule watakazopangiwa nasi vinginevyo. Ni imani yangu walimu wapya wote watakuwa tayari kufanya kazi maeneo yenye mahitaji. Orodha rasmi ya walimu na vituo watakavyokuwa wamepangiwa itapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –OWM TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 25/4/2015.
                                        IMETOLEWA NA JUMANNE A. SAGINI
                                           KATIBU MKUU OWM –TAMISEMI
                                                 TAREHE 13/04/201

Hakuna maoni: