Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 20 Machi 2014

Soma magazeti yote ya Tanzania katika Kurasa kupitia http://bwandustephano.blogspot.com/

Soma magazeti yote ya Tanzania kupitia 'Kurasa' katika BWANDU"S BLOG ama bofya http://bwandustephano.blogspot.com/ mda wote utapata habari juu ya kitu chochote.

Jumanne, 11 Machi 2014

Academic question,,try to answer it.
Arsenal Vs Bayern

Unaweza kubashiri ni nani ataibuka mshindi leo? ni swali gumu sana washabiki wengi wa Arsenal wanajiuliza na majibu hawana, ila wanamatumaini kuwa huenda Mungu wao atawapeperushia upepo wa bahati na wataifunga Bayern,, ila sijui kama itakuwa hivi,,tusubiri 90dk. 

Mjadala Bungeni wa kujadili rasimu ya pili ya katiba.

Ni siku kadhaa sasa bunge maalum la katiba laendelea bungeni Dodoma, na huku wananchi hatuoni maendeleo yoyote isipokuwa malumbano tu kati ya wajumbe wa bunge hilo. Ni dhahiri kuwa, tumechoshwa na malumbano yasiyokuwa na faida kwa watanzania, na huku wakipoteza ama kuongeza siku nyingi kujadili mambo yasiyokuwa na msingi huku wakila posho zitokanazo na jasho la watanzania. Ombi langu kwa serikali, kama waheshimiwa wabunge wameshindwa kufikia makubaliano juu ya Maada yao nyepesi sana (kwao wajumbe wa bunge maalum wakiliona jambo zito), basi Mh. Rais avunje bunge hilo,kwani pesa ya umma inazidi kupotea pasipo faida.. Ama ilitakiwa jopo la Mh. sana Warioba, likae na lipitishe rasimu ile kwa wananchi tuipigie kura, na sio wabunge.

Ijumaa, 28 Februari 2014

Picha za UDOM


YOU'RE WELCOME 2 UDOM


Orodha ya vyuo vikuu bora Tanzania, 2014.Hii ni orodha ya vyuo vikuu bora Tanzania mwaka huu 2014.
source;http://www.4icu.org/tz/
University Sort by University name

 University of Dar es Salaam
Dar es Salaam ...
 Sokoine University of Agriculture
Morogoro ...
 The Hubert Kairuki Memorial University
Dar es Salaam
 Tumaini University Makumira
Arusha
 Muhimbili University of Health and Allied Sciences
Dar es salaam
 St. Augustine University of Tanzania
Mwanza ...
 Ardhi University
Dar es Salaam
 Catholic University of Health and Allied Sciences
Bugando
 Nelson Mandela African Institution of Science and Technology
Arusha
10  Mzumbe University
Morogoro
11  The University of Dodoma
Dodoma
12  Mount Meru University
Arusha
13  St. John's University of Tanzania
Dodoma
14  The State University of Zanzibar
Zanzibar City ...
15  Teofilo Kisanji University
Mbeya
16  Sebastian Kolowa Memorial University
Lushoto
17  Zanzibar University
Zanzibar City
18  The University of Arusha
Arusha
19  Muslim University of Morogoro
Morogoro
20  Mbeya University of Science and Technology
Mbeya
21  St. Joseph University in Tanzania
Mbezi Luguruni
22  International Medical and Technological University
Dar es Salaam
23  United African University of Tanzania
Dar-es-Salaam
24  University of Bagamoyo
Dar es Salaam
25  Eckernforde Tanga University
Tanga
Source;  http://www.4icu.org/tz/

Katika orodha hii, napenda kukipongeza chuo kikuu cha Dar es salaam kwa kuendelea kuongoza kwa ubora katika vyuo vyote Tanzania, ingawa kwa upande wa Africa top 100 universities UDSM ni cha 12.

Pia nafurahi kuona chuo kikuu kichanga sana Tanzania,THE UNIVERSITY OF DODOMA (UDOM), kinakimbizana na baadhi ya vyuo vikuu vikongwe hapa nchini. Hii ni dhahiri kuwa, kasi ya UDOM ni kubwa ukilinganisha umri wake wa uwanzishwaji wa chuo, ambapo kimeanzishwa mwaka 2007. Hivo kina umri wa miaka 6.5-7, wakati vyuo vingine vina zaidi ya miaka 20-40s

Hoja ya Mh. Mbatia yamkuna mwenekiti wa mda Mh. Pandu Ameir Kificho wa bunge maalum la katiba

Ilikuwa ni hoja ya kibusara ambayo ilichangiwa na Mh. Mbatia wakati wa Taswira ya Bunge maalum hapo jana. Mh. Mbatia aliwasihi wajumbe wote kutumia hekima na busara katika kuendesha na kutoa maoni juu ya uchambuzi wa rasimu ya pili ya katiba. Aliwaomba wajumbe kuwa na focus ya pamoja na kuacha malumbano yasiyojenga umoja ndani ya wajumbe, kwani alidai kuwa wajumbe wako pale kwa kazi ya kuchambua katiba ya watanzania wote na sio kwa maslahi ya vyama vya siasa na makundi ya kidini. 

Hoja hiyo ilimgusa mwenyekiti wa mda Mh. Pandu na kuwasihi wajumbe wote kuufanyia kazi ushauri huo.

Picha hizi baadhi ya wajumbe waliochangia hoja jana, bungeni kwenye semina hiyo.Mjadala bungeni juu ya Rasimu ya pili ya katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tz

Jana tarehe 27.2.2014 ilikuwa ni siku nyingine ambapo wabunge maalum wa bunge la katiba mpya wamejadiliana juu ya sheria na taratibu za kuliongoza bunge maalum wakati wa shughuli nzito ya kuchambua na kuandaa katiba mpya.

Baadhi ya wajumbe walishiriki kutoa maoni, mapendekezo ya nikwa namna gani mchakato mzima wa shughuli bungeni ziendeshwe. Katika hoja na mitizamo mingi ya wabunge ilionekana kutofautiana juu ya kipengele cha kupiga kura baada ya makusanyo, mapendekezo na mapitisho ya mijadara na maoni ya wajumbe wote bungeni kupitia kamati maalum iliyoteuliwa na bunge kushughurikia maoni na mapenekezo ya wabunge.
 
Katika tofauti za hoja za wabunge, baadhi walionekana kuunga mkono kura za siri na huku wengine wakipendekeza kura za wazi (dhahiri). Mbali na hayo, katika utoaji wa hoza hizo kinzani, baadhi ya wajumbe walionekana kutoa hoja zao kwa hisia kali na kana kwamba wanatishiana.

Lakini kwa mantiki ya kawaida, kulingana na mchakato mzima wa kuchambua rasimu hiyo inaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia na inafanyika pasipo na usiri wowote, kwani mijadara huoneshwa kwenye vyo mbalimbali vya habari, itakuwa vyema endapo kura zitapigwa dhahiri (wazi). Na mantiki ya kudai kwamba kura zipigwe kwa usiri kama walivodai baadhi ya wajumbe wa bunge, kuwa ni utaratibu wa mda mrefu na kila bunge la katiba kokote duniani hufanya vile, nadhani sio razima sana, kwani sisi watanzania tunataka kuona wajumbe wapige kura dhahiri pasipo kuogopa mtu mwingine ili kuweza kukomaza demokrasia ndani ya Nchi yetu toka bungeni na kwa Nchi nzima

Jumanne, 25 Februari 2014

KANDANDA-DUNIANI

NI KLABU BINGWA ULAYA (UEFA)
Leo kivumbi kingine kutimka uwani huko Ugiriki kati ya klabu ya timu ya nchi hiyo..Olympiakos Vs Manchester United kutoka Uingereza,,
Ndugu mwanasoka na mpenzi wa mpira,, ni uwanja wako wa kutabiri nani atashinda mchezo huo,,
unaweza ku-like page hii, ama kutoa maoni yako

Wanafunzi wa kiume wauwawa, huko Nigeria

Ni katika jimbo la Yobe huko Nigeria ambapo wanafunzi wa kiume wameuwawa na jeshi la waasi la Boko haramu ambalo linasadikika kuwa ni tawi la Alqaeda. Taarifa hizi zimebainishwa na jeshi la police la Nigeria baada ya tukio hilo katka jimbo la Yobe.


Rais wa mpito,Ukraine atoa onyo

Rais wa mpito (interim president) wa Ukraine Mr. Olexander Turchynov aonya juu ya tishio la kusambaratika kwa nchi yake kufuatia kuondolewa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Bw. Victor Yamkovych
  

Jumapili, 23 Februari 2014

Taarifa za wiki hii, Duniani kote


          Picha hapo juu; ni Mh. Dk. J. Kikwete akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Misri
 

 Picha hapa chini:  Simba yashindwa kufurukuta mbele ya JKT Ruvu leo baada ya kuogeshwa goli 3-2 katika uwanja wa Taifa leo      

Dkt. Magufuri atembelea kwenye tukio.