Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 22 Machi 2015

ZITTO KABWE;- ATIMKIA CHAMA KIPYA CHA 'ACT' NA ATAJA SABABU TANO ZA KUHAMIA CHAMA HICHO BAADA YA KUNG'ATUKA KUTOKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

 Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ametaja sababu tano za kujiunga na chama cha ACT-Tanzania huku akijigamba kuwa yeye ni mchapakazi na kwamba sasa mambo yote ni mbele kwa mbele.
Akimnukuu Rais wa zamani wa Ghana, Hayati Kwame Nkrumah aliyewahi kusema, ‘forward forever, backward never’, jana Zitto alisema, sasa ni wakati wa kuangalia mbele, hakuna kurudi nyuma tena huku akijisifu kwa umahiri wake katika kazi.
“Mimi ni mchapakazi…siangalii nyuma tena, naangalia mbele . Mapambano yanaanza matokea mtayaona baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,”alisema Zitto kujiamini.
Zitto ambaye aling’atuka kutoka kwenye nafasi ya Ubunge  Ijumaa iliyopita kupitia Chadema na kujiunga na chama ACT siku moja baadae, alisema watu wengi wamekuwa nini kingefuata baada ya ya kuachia nafasi .
“Sasa napenda kuwaarifu kuwa Machi 20, mwaka huu siku ya Jumamosi nilijiunga na chama cha ACT na kukabidhiwa kadi ya uanachama na mwenyekiti ACT,  Tawi la Tegeta.
Hii ilikuwa moja katika siku muhimu kabisa katika maisha yangu ya kisiasa,”alisema Zitto na kuongeza kuwa amelipa ada ya uanchama hadi mwaka 2025.
Zitto ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alifunguka na kueleza sababu za kuhamia katika chama hicho ambacho kimenzishwa juzi na siyo chama kingine cha siasa, kama ambavyo watu wengi wanajiuliza.
“Nimejiunga na ACT  kwa sababu ninaona kwamba huku ndiko kunakaoendana na kile ambacho mimi nimekipigania kwa miaka yote tangu nianze siasa, ambacho nikuweka maslahi ya taifa mbele dhidi ya kitu kingine chochote,”alisema Zitto huku akishangiliwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliohudhuri mkutano huko.
Alisema sababu nyingine ni kwamba ACT ni chama pekee nchini kinachokubaliana na Itikadi ya Ujamaa na kinaamini katika Falsafa ya Unyerere.
Aliongeza kuwa, amejiunga na chama hicho kwa sababu ni chama kinachoamini katika msingi wa uadilifu na kimeweka miiko ya maadili ya uongozi katika kuhakikisha kwamba viongozi wote wa ACT wanakubaliana nayo na wanaisaini.
“Naamini kuwa na miiko na maadili kwa viongozi ni mwanzo wa kuhakikisha kwamba jamii yetu inaishi katika uadilifu na kwamba viongozi wanakuwa na audilifu katika jamii,”alisema.
Aliongeza; “Mtakumbuka kwamba katika miaka yangu yote ya ubunge nimepigania uwajibikaji na uwazi. Hii ni misingi ambayo ninaamini kwamba  ni moyo wa utashi na umma,” NANI MKALI KATI YA LIVERPOOL DHIDI YA MANCHESTER UNITED LEO @ 13:30 GMT 
SAFARI ZA TRENI KUANZA TENA TAREHE 24 MARCH, 2015.


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unafuraha kuwataarifu  abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa huduma ya treni ya abiria itaanza upya hapo siku ya Jumanne Machi 24, 2015 kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam saa 11 jioni.
Wananchi wanaotaka kusafiri wafike stesheni zilizo karibu yao kwa ajili ya kukata tiketi ya safari hiyo.
Huduma ya usafiri wa reli ilisitishwa wiki mbili zilizopita Machi 6, 2015 baada ya eneo la tuta la  reli kati ya Stesheni za Kilosa na Kidete kukuharibiwa vibaya...


Mp. Peter Msigwa ndani ya mjengo na hoja zake kali dhidi ya Serikali ya TZ...........

Jumamosi, 21 Machi 2015


 


NI MAPINDUNZI KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI TANZANIA KATIKA AZIMA YA KUFIKIA MPANGO WA 'BIG RESULTS NOW'........ NI MABEHEWA MAPYA YALIYONUNULIWA KUTOKA KOREA KWA AJILI YA KUTUMIKA KATIKA RELI YA KATI,,,,TOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA;

WAZIRI MKUU PINDA, MIZENGO; AKIKAGUA MOJA YA JIKO LA UMEME LA KUPIKIA NDANI YA BEHEWA LA 2nd CLASS- ZILIZONUNULIWA TOKA KOREA;WIZIRI MKUU AKIONGOZANA NA WAZIRI WA WIZARA YA UCHUKUZI TZ
PG4A2797PG4A2800

NI MUONEKANO NDANI YA MABEHEWA MAPYA YA TRENI;PG4A2808

Ijumaa, 20 Machi 2015


 
 
 
 Mh. Zitto Zuberi Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini
Mheshimiwa Spika, nilijiunga na Bunge lako tukufu mwaka 2005 nikiwa kijana mdogo mwenye malengo ya kupaza sauti ya vijana kwenye masuala yanayohusu nchi yetu na pia kutetea maslahi ya wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma.

Katika kudumu kwangu kama mbunge nililelewa na kukuzwa na chama cha siasa cha CHADEMA ambacho kupitia chama hiki niliingia Bungeni. Chama hiki kilinilea na kunikuza tangu nikiwa na umri wa miaka 16 na kupitia chama hiki nimejifunza mambo mengi sana. Nimeijua nchi yangu, nimejua siasa na nimejulikana ndani na nje ya nchi. Nitakuwa mwizi wa fadhila nisipotoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa CHADEMA na viongozi ambao nimefanya nao kazi muda wote nikiwa mwanachama na kiongozi.

Mheshimiwa Spika, Chama kilinikuza kama mwanasiasa lakini watu wa Kigoma Kaskazini ndio walionipa kiti hiki ninachokalia kama Mbunge. Juzi nilipokuwa nyumbani nilipata fursa ya kuwashukuru rasmi wananchi kwa imani waliyonipa kuwatumikia kwa vipindi viwili mfululizo. Wengi wenu ndugu zangu wabunge mnafahamu, mihula miwili sio jambo la mchezo, sio lelemama. Mola atawalipa wananchi wa Kigoma kwa imani kubwa walioionyesha kwangu na kuniwezesha kulitumikia Taifa langu kwa namna nilivyolitumikia.

Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii leo kuzungumzia suala la muda mrefu sasa la kutoelewana kati yangu na chama changu na hivyo kuleta msuguano kati ya wananchi walionichagua kuwawakilisha na chama nilichopitia na kupeperusha bendera yake wakati wa uchaguzi mkuu.

Licha ya msimamo wangu wa siku zote kwamba wananchi pekee waliomchagua mwakilishi wao ndio wawe na mamlaka ya kumwondoa kwenye uwakilishi mchaguliwa huyo, mfumo wetu wa kikatiba na mfumo wetu wa kisiasa haupo hivyo na umeamua vinginevyo.

Mheshimiwa Spika, kwamba chama cha siasa kinaweza kumvua uanachama mwanachama wake na hivyo kupoteza kiti chake cha uwakilishi wa wananchi wake ni moja ya makosa makubwa ya kikatiba ambayo tumeendelea kuyakumbatia, nimekuwa nikipinga na nitaendelea kupinga udikteta wa vyama dhidi ya utashi wa wananchi.

Mheshimiwa Spika, licha ya upinzani wangu mkali wa vifungu kandamizi vya kikatiba, kama mzalendo ninaiheshimu Katiba yetu na mfumo wetu wa sasa na ninaheshimu uamuzi wa mahakama dhidi ya kesi yangu na sitakata rufaa. Hatua itakayofuata ni uamuzi wa chama changu na baadhi ya viongozi wameshatangaza kwa umma kupitia vyombo vya habari kunivua uanachama ingawa sijapewa taarifa rasmi.

Mheshimiwa Spika, ningeweza kukata rufaa kuhusu maamuzi ya mahakama kwani kuna sababu lukuki ya kushinda rufaa hiyo. Lakini ninadhani nimepigania haki zangu kwa muda mrefu sasa. Nimepigania kupanua wigo wa demokrasia ndani ya chama changu kwa muda mrefu sasa. Lakini ugomvi huu hauna manufaa kwa pande zote husika, kwa hakika unatuumiza wote.

Mimi ni mwanademokrasia. Naamini katika siasa za ushindani ndani ya chama na katika mfumo mzima wa siasa kitaifa. Lakini sitakuwa tayari kudhoofisha harakati na kazi kubwa walizofanya wanamageuzi waliotutangulia kwa kuendeleza ugomvi unaotuumiza. Hivyo niko tayari kukubali kukaa pembeni. Ninaamini kuwa mapambano ya kuleta mabadiliko ya kweli na demokrasia katika nchi yetu Tanzania ni makubwa kuliko mimi, kuliko kiongozi yoyote wa Chadema na kuliko wanachama wa Chadema.

Mapambano haya ya mabadiliko si kwa ajili ya kizazi hiki tu bali kwa vizazi vijavyo. Ndiyo maana siku zote nimesema Nchi kwanza, vyama baadae. Kuona makundi yanajitokeza ndani ya harakati hizi, na kuwa na uhasama mkubwa uliopindukia, unawakatisha tamaa wananchi wanaotutumaini kuleta siasa iliyo tofauti na siasa za sasa. Muda umefika wa kupiga mstari na kuanza upya. Hivyo nimeamua kuwa nitatii maamuzi ya chama ya kunivua uanachama na kung’atuka ubunge.

Mheshimiwa Spika, naomba niweke wazi kuwa nimefikia uamuzi huu kwa utashi wangu mwenyewe na nimepewa Baraka zote na wananchi wangu na wazee wa Jimbo la Kigoma Kaskazini. Najua Watanzania wengi ambao nimewatumikia kwa moyo wangu wote katika kipindi cha miaka hii 10 wanaweza wasikubaliane na uamuzi huu.

Hata hivyo Watanzania wajue kuwa mfumo wetu wa siasa na katiba unatoa nguvu kwa vyama vya siasa kudhibiti wabunge wake. Naamua hivi kwa sababu wenzangu ndani ya chama ambao nimehangaika nao usiku na mchana kujenga chama na kukifisha hapa kilipo hawapo tayari kufanya kazi tena na mimi.

Nimesoma na kusikia kauli nyingi zinazoweka wazi kuwa hawanitaki ndani ya chama. Nimejitahidi kwa njia zangu zote kuona kama tunaweza kuendelea kufanya kazi pamoja ya kujenga mfumo madhubuti wa vyama vingi nchini lakini imekuwa ngumu kama mwanachama mwenzao. Ninaheshimu uamuzi wao huo.

Mheshimiwa Spika, kwa miaka kumi hii si yote niliyafanya sahihi, yapo ambayo niliyakosea kama mwanadamu katika kufanya kazi kwangu, kwa namna yeyote ile naomba radhi Watanzania wote kwa yote ambayo sikuyafanya kwa usahihi. Mimi ni binadamu, kiumbe dhaifu, sijakamilika. Ni Mola peke yake amekamilika.

Mheshimiwa Spika, siwezi kuanza maisha yangu mapya bila ya kulishukuru Bunge lako tukufu, Bunge la Tisa chini ya Mzee Samwel Sitta na Bunge la Kumi chini yako Mama Anna Simamba Makinda. Bunge limekuwa ni nyumbani kwangu kwa takribani muongo mmoja. Nimekuzwa, nimejifunza, nimepambana, nimefurahi na nimelia ndani ya Bunge hili. Kwa pamoja tumepigania maslahi ya wananchi wetu na kupingana na kufanya mambo kwa mazoea na hivyo kuleta mabadiliko kadhaa. Ni kipindi hiki ambapo wabunge tumekuwa na sauti, Bunge la Tisa lilijenga ‘Bunge lenye Meno’ katika kupambana na ufisadi. Bunge la Kumi limejenga ‘Bunge lenye nguvu’ katika mfumo wa Bajeti ya nchi yetu. Kupitia Bunge hili tumeweka misingi ya kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, wakati Bunge la Tisa litakumbukwa kwa hoja ya Buzwagi iliyopelekea nchi yetu kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa uendeshaji wa sekta ya madini (Sera mpya ya Madini na Sheria mpya ya Madini ) na hivyo mapato ya sekta ya madini kuongezeka kutoka Tshs 32 bilioni kwa mwaka mpaka Tshs 450 bilioni kwa mwaka hivi sasa; Bunge la Kumi litakumbukwa kwa hoja maalumu ya Tegeta Escrow iliyopelekea mfumo wetu wa maadili ya Viongozi kupitia Baraza la Maadili kuanza kufanya kazi kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa katika miaka iliyopita. Mimi kuwa sehemu ya mabunge yaliyotekeleza hatua hizo za mabadiliko ni jambo la kujivunia sana.

Mheshimiwa Spika, kwa familia yangu, wajumbe wa PAC, tumekuwa nguzo kubwa ya kujenga uwajibikaji wa Serikali kwa Bunge na wananchi. Napenda kuwashukuru kwa dhati kabisa kwa kuniunga mkono na kwa kunipa ushirikiano kama Mwenyekiti wao. Changamoto na malezi mliyonipa kwa miaka yote hii yamejenga Mtanzania mmoja mwenye dhati ya kuitumikia nchi yake, muda wowote, wakati wowote na kwa namna yeyote ile bila woga wala upendeleo. Nawashukuru kwa kujitoa kwenu kwa nchi yetu na dhamira isiyo na mawaa ya kujenga Taifa imara zaidi.

Nitaendelea kuwatumikia wananchi wa Kigoma Kaskazini na Taifa langu hata kama nimelazimika kuachia nafasi yangu ya ubunge kwa kipindi hiki kilichosalia kwa kusimamia ukweli, kutetea demokrasia ya kweli na kupigania maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida bila ubaguzi wowote.

Mheshimiwa Spika, Kwa CHADEMA, licha ya tofauti zetu ambazo zimekua kiwango cha kutosameheka, najivunia kwa fursa mliyonipa kuwa sehemu ya Baraza hili la Taifa ambalo leo ninalihutubia kwa mara ya mwisho kama mbunge wa Kigoma Kaskazini. Fursa iliyonifanya niweze kuitumikia nchi yangu na mkoa wangu wa Kigoma. Inawezekana tusiweze kuelewana katika masuala ya uongozi, misingi na itikadi, lakini ninaamini tunapaswa kuelewana na kukubaliana katika kubwa ya kuijenga nchi yetu kuwa Taifa linalojitegemea na lisilo na aina yeyote ya ubaguzi. Taifa lenye uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira na kuondoa umasikini, ujinga na maradhi, Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ni matumaini yangu kuwa tutakuwa bega kwa bega katika harakati hizi katika siku zijazo. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, nafasi hii ya kihistoria tuliyopewa haihitaji siasa za ubinafsi na unafsi! Uzalendo wetu utapimwa kwa uwezo wetu wa kuweka tofauti zetu binafsi pembeni kwa lengo lililo kubwa zaidi yetu.

Mheshimiwa Spika, Mwisho kwa wananchi wa Jimbo langu, wana Kigoma na raia wote wa Tanzania ambao kwa ridhaa yao nimekaa katika viti hivi kwa miaka takribani kumi, nawahakikishia kuwa dhamira yangu kuwatumikia, nia yangu na sababu za kutoa utumishi wangu kwenu vimekuwa na nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Huu ni mwanzo mpya. Ngugi aliandika ‘a grain of wheat’ kwa maana ya kwamba ‘Ili Mbegu iweze kumea lazima ife kwanza’.
Asanteni sana.

Jumatatu, 14 Aprili 2014

The relief of your life is placed in your hands now..Its all about changing your life and make money by joining the Excellent initiated NGO in Tz..for more details, just click http://www.truevisiontz.blogspot.com
   'Let us change Tanzania and Africa at large..'

Alhamisi, 20 Machi 2014

Soma magazeti yote ya Tanzania katika Kurasa kupitia http://bwandustephano.blogspot.com/

Soma magazeti yote ya Tanzania kupitia 'Kurasa' katika BWANDU"S BLOG ama bofya http://bwandustephano.blogspot.com/ mda wote utapata habari juu ya kitu chochote.

Jumanne, 11 Machi 2014

Academic question,,try to answer it.
Arsenal Vs Bayern

Unaweza kubashiri ni nani ataibuka mshindi leo? ni swali gumu sana washabiki wengi wa Arsenal wanajiuliza na majibu hawana, ila wanamatumaini kuwa huenda Mungu wao atawapeperushia upepo wa bahati na wataifunga Bayern,, ila sijui kama itakuwa hivi,,tusubiri 90dk. 

Mjadala Bungeni wa kujadili rasimu ya pili ya katiba.

Ni siku kadhaa sasa bunge maalum la katiba laendelea bungeni Dodoma, na huku wananchi hatuoni maendeleo yoyote isipokuwa malumbano tu kati ya wajumbe wa bunge hilo. Ni dhahiri kuwa, tumechoshwa na malumbano yasiyokuwa na faida kwa watanzania, na huku wakipoteza ama kuongeza siku nyingi kujadili mambo yasiyokuwa na msingi huku wakila posho zitokanazo na jasho la watanzania. Ombi langu kwa serikali, kama waheshimiwa wabunge wameshindwa kufikia makubaliano juu ya Maada yao nyepesi sana (kwao wajumbe wa bunge maalum wakiliona jambo zito), basi Mh. Rais avunje bunge hilo,kwani pesa ya umma inazidi kupotea pasipo faida.. Ama ilitakiwa jopo la Mh. sana Warioba, likae na lipitishe rasimu ile kwa wananchi tuipigie kura, na sio wabunge.

Ijumaa, 28 Februari 2014

Picha za UDOM


YOU'RE WELCOME 2 UDOM


Orodha ya vyuo vikuu bora Tanzania, 2014.Hii ni orodha ya vyuo vikuu bora Tanzania mwaka huu 2014.
source;http://www.4icu.org/tz/
University Sort by University name

 University of Dar es Salaam
Dar es Salaam ...
 Sokoine University of Agriculture
Morogoro ...
 The Hubert Kairuki Memorial University
Dar es Salaam
 Tumaini University Makumira
Arusha
 Muhimbili University of Health and Allied Sciences
Dar es salaam
 St. Augustine University of Tanzania
Mwanza ...
 Ardhi University
Dar es Salaam
 Catholic University of Health and Allied Sciences
Bugando
 Nelson Mandela African Institution of Science and Technology
Arusha
10  Mzumbe University
Morogoro
11  The University of Dodoma
Dodoma
12  Mount Meru University
Arusha
13  St. John's University of Tanzania
Dodoma
14  The State University of Zanzibar
Zanzibar City ...
15  Teofilo Kisanji University
Mbeya
16  Sebastian Kolowa Memorial University
Lushoto
17  Zanzibar University
Zanzibar City
18  The University of Arusha
Arusha
19  Muslim University of Morogoro
Morogoro
20  Mbeya University of Science and Technology
Mbeya
21  St. Joseph University in Tanzania
Mbezi Luguruni
22  International Medical and Technological University
Dar es Salaam
23  United African University of Tanzania
Dar-es-Salaam
24  University of Bagamoyo
Dar es Salaam
25  Eckernforde Tanga University
Tanga
Source;  http://www.4icu.org/tz/

Katika orodha hii, napenda kukipongeza chuo kikuu cha Dar es salaam kwa kuendelea kuongoza kwa ubora katika vyuo vyote Tanzania, ingawa kwa upande wa Africa top 100 universities UDSM ni cha 12.

Pia nafurahi kuona chuo kikuu kichanga sana Tanzania,THE UNIVERSITY OF DODOMA (UDOM), kinakimbizana na baadhi ya vyuo vikuu vikongwe hapa nchini. Hii ni dhahiri kuwa, kasi ya UDOM ni kubwa ukilinganisha umri wake wa uwanzishwaji wa chuo, ambapo kimeanzishwa mwaka 2007. Hivo kina umri wa miaka 6.5-7, wakati vyuo vingine vina zaidi ya miaka 20-40s